HAKI NA AMANI
Haki na amani kwa namna moja au nyingine huitwa maneno pacha ingawa kila neno linaweza kuwa na maana tofauti na jingine.
Neno haki kwa tafsiri au maana ya kawaida ni stahiki ya mtu kwa maana ya kile mtu astahilicho mtu kwa minajili ya kuwa binadamu au vinginevyo kama ilivyoainishwa katika jamii husika.
Hii ni kusema kwamba zipo haki kama vile za kisiasa, kiuchumi, kijamii na nyingine nyingi kuendana na jamii yenyewe inavyoweza kuainisha kulingana na mahitaji katika jamii hiyo husika.
Haki ya mtu au watu ikipokonywa au kuminywa mara moja hujibainisha kwamba hapa kuna jamba ambalo limekwenda kinyume. Madhara ya hili huwa kubwa kuliko hata gharama ya kuandaa haki hiyo.
Ni madhila ya Haki ndiyo yanayotupatia Amani, kwamba palipo na Haki pana Amani. Kwa mantiki hii Amani ni zao la Haki. Neno amani lina dhana pan asana kwani inatiririka kutoka kwa mtummoja mmoja , kundi dogo la watu hadi jamii zima kwa ujumla wake.
Kwa upande mwingine tunaweza kusema Haki huzaa imani na Imani huzaa Amani. Watu waliotendewa Haki, wasio na hofu Haki zao kufinyangwa, huwa na imani thabiti dhidi ya mamlaka zinazokabidhiwa jukumu la kutoa Haki hiyo.
Hapa ndipo tunapoona upacha kati ya Haki na Amani, kwamba jamii iliyo na uhakika wa kupatiwa Haki zake itakuwa na Amani, na palipo na Amani ndipo maendeleo huwepo!
Swali la kujiuliza hapa ni: je, jamii zetu zinapata Haki zake kwa kadri ya mahitaji yao? Amani ipo? Na kama ipo ni kwa kiwango gani? Kama haipo, ni kwa nini?
Na je, kama wana jamii tunacho chochote cha kuchangia ili Haki na Amani viwepo? Tunashiriki vipi katika upatikanaji wake pasipo jamii kuparaganyika?
Maswali yote haya na mengine mengi yanahitaji mjadala mpana kwa kila aliyepewa pumzi ya uhai na Mwanyezi Mungu kwa karama zake, wawe ni: wananzuoni au wanagenzi au wakurugenzi.
Pengine kutokana na uzito na upana wa mjadala huu, ningependa niseme kila mmoja wetu ahusike ili tuweze kujifunza kwa pamoja na tuone jamii yetu inakwenda wapi na ipo katika hali ipi.
Upo usemi usemao Haki yako inapoishia ndipo haki ya mwenzi inapoanzia
Tujue kwamba kukosekana kwa Haki kumechangia sana kuongezeka kwa umaskini nchini mwetu.
Fikiri kwa mfano, mwanafunzi wa elimu ya juu anahitaji mkopo. Katika fomu anayojanza, anatkiwa kugongewa mhuri mahakani.
Anapofika mahakani anamkuta karani na kuambiwa kuwa inatakiwa igongwe mihuri sita na kila mhuri ni Tsh 1500. Huyu mwanafunzi anagongewa na hapewe risiti kuonyesha hiyo fedha inaingia kwenye mfuko wa nani.
Au pia huyo mwanafunzi anashindwa kupata hiyo fedha na anaondoka. Na hivyo anaendelea kuhangaika maana bodi ya mikopo haitoi fedha kwa kuwa mwanafunzi huyo hakufanikiwa kigonga mhuri katika fomu huko mahakani. Je, huyu atakuwa na amani?
Hivi ni nani alitakiwa ahakikishe kule mahakamani mambo yanaenda sawa. Siyo serkali yetu?
Kwa kweli ndugu zangu pasipo na haki hakuna maendeleo yatakuwepo.
Rushwa ikitawala, hakuna raia atapata haki yake. Hakuna mtu atakuwa na imani na mtawala wake.
Kinachohitajika hapa ni mabadiliko makubwa katika uendeshaji wa masuala ya umma. Kama kuna wakati mtu aliyeonwa na kashfa ya kuchukua rushwa anataka tena achaguliwe awe kiongozi, na anachaguliwa, hivi kweli watu wa jamii hiyo wataonekana makini katika mamabo yao au wanafanya mchezo!!
Hapa ndipo mgogoro wa upatikanaji wa haki na Amani katika jamii zetu unapoanzia: kwamba waliokabidhiwa keki ya taifa ili waigawe kwa Haki, humegeanamegeana. Sehemu kubwa ya keki hiyo huichukua wao wenyewe kwa manufaa yao na familia zao.
Nimalinze kwa kusema Haki na Amani si swala la utashi, ni la lazima ili tuweze kupata ustawi wa kweli wa jamii zetu ili kutimiza usemi usemao: “Dunia unaweza kuitafsiri utakavyo wewe, lakini kinachotakiwa ni maendeleo”.
2 comments:
nakukubali sana mwl. hongera kwa makala nzuri hebu itoe kwenye gazeti mojawapo watu wasome. kuna marekebisho machache tu ya spelling na space ukiwa na mtu aisome karibu uirekebishe. Lakini pia nikupe hongera kwa kufungua website, kwani najua si kazi rahisi nakutakia mafanikio mema.
Mwl. kwa ujumla nimeipenda sana kazi yako, nilikuwa nashauri kama table ya YALIYOMO ikakaa kwenye top page kabisa ili msomaji ajue ndani kuna nini akifungua tu hii blog. itasaidia na kuvutia mtu kwanza nini kilichomo na pia atajipanga aanzie wapi kusoma. kazi nzuri sana mwl.
Post a Comment