Saturday, June 28, 2014

HABARI NJEMA KWA WAFUGAJI WA KUKU NA NDEGE WA AINA ZOTE

Ndugu wapendwa wajasiriamali wenzangu, napenda kuwashirikisha jambo hili muhimu ambalo tukilizingatia kwa akili zetu zote na nguvu zetu zote huku tukimshirikisha Muumba wetu atujalie afya tele tunaweza kuondokana na madhila haya ya umaskini.
FikiriMungu amekujalia tabia ya ujasiriamali na wewe ukachagua kufuga kuku tuseme kuku wa kienyeji.
Katika harakati zako ukabahatika kununua mashine ya kuangua vifaranga (incubator). Tuseme mashine hiyo inabeba mayai elfu moja na ni nzuri imetoka kwa fundi aliyebobea maana kwa busara kabla ya kununua imefanya utafiti uone nani fundi kweli na mashine zake zina ufanisi mkubwa.
Baada ya kupata mashine umenunua mayai ya Tsh. 350000. Unaweka kwenye mashine yako unapata labda tuseme vifaranga 850. Kuangalia unakuta mashine yako imetumia umeme wa Tsh 50000. Umetafuta wateja wa vifaranga wako ukapata na vyote vikachukuliwa kwa kila kimoja Tsh. 2000 maana katika eneo lako hiyo ndo bei. Kihesabu hapo utakuwa umetapata Tsh. 1700000. Ukitoa Tsh 350000 uliyonunulia mayai na Tsh. 50000 ya umeme unabaki na kiasi gani ndugu mjasiriamali? Mimi situmii calculator hapa ila natumia uzoefu wa kitu ambacho nimekifanya kabisa na kwangu Tsh. 1400000 inabaki mfukoni kama faida.
Sasa ndugu mjasiriamali unangoja nini? Njoo tuongee kwa pamoja tuondokane na unyonge huu kwa kufanya kazi halali ambayo haina manung'uniko yoyote.
USHAURI NI KUWA USIJARIBU KUNUNUA MASHINE ZA KUANGUA VIFARANGA KABLA HUJAFANYA UTAFITI UKAONA UFANISI WA HIZO MASHINE.
HABARI NJEMA KWA WAJASIRIAMALI
Kwa sasa tunatengeneza mashine za kuangua vifaranga zaukubwa mbalimbali kama ifuatavyo:
1. Mashine za mayai 90 = Tsh. 600,000/
2. Mashine za mayai 120 = Tsh 800,000/
3. Mashine za mayai 180 =Tsh. 1,500,000/
4. Mashine za mayai 300 =Tsh. 2,200,000/
5. Mashine za mayai 600 =Tsh. 2,800,000/
6. Mashine za mayai 1000 = Tsh. 3,500,000/
 Mashine zetu zina sifa nzuri sana za uanguaji mzuri wa mayai. Mnakaribishwa wote mfike mjionee zinavyofanya kazi. Sisi tupo Iringa mjini. Mnakaribishwa sana.