image slider

HUDUMA TUNAZOZITOA
Watengenezaji wa mashine za kuangulia vifaranga vya kuku
Wauzaji wa vifaranga vya kuku
Ushauri wa ufugaji wa kuku
Mashine za kuangulia vifaranga vya kuku
Wauzaji wa vifaranga vya kuku
Mashine za kuangulia vifaranga vya kuku

Monday, December 7, 2015

VIFARANGA VIFARANGA VIFARANGA

Tunawakaribisha wateja wetu wote kujipatia vifaranga vya bata mzinga. Mjini Iringa
Namba zetu ni 0753903809

Wednesday, July 1, 2015

UFUGAJI WA KUKU KWA FAIDA NA TIJA

Wajasiriamali wengi hupenda miradi ambayo huwaletea matokeo au faida mapema,
Mradi wa kufuga kuku ni mradi ambao huleta faida kwa muda mfupi sana.
Ili upate faida kubwa ni vizuri ukawa na mradi ambao unaweza kuumudu kwa kuwa na mahitaji muhimu katika mradi wako.
MFANO, mtu anayetaka kufuga kuku tuseme 500 anatakiwa kuwa na vifaranga 550. Awe ana uwezo wa kuwalisha hao vifaranga na kuwapa tiba. Pia awe na uwezo wa kujenga banda bora.

 Baada ya hapo kinachotakiwa ni umakini wa kufuatilia mradi katika kipengele cha utoaji huduma kwa kuku hao. Katika kundi hilo la kuku 500, 50 wanatakiwa kuwa majogoo na 450 mitetea.
Katika hao mitetea 450 aslimia 75 wanatakiwa watage kila siku. Asilimia 75 ya 450 ni kuku 337. 
Mayai ya kuku hawa huuzwa kwa Tsh. 300@. Hivyo kila siku utapata Tsh 337 x 300 = Tsh. 100000.
Kama mtu anaweza kupata Tsh. 100000 kila siku kwa mwezi una uhakika angalau wa kuweka akiba ya Tsh. 100000 bila shida. Kama utaweka akiba ya fedha hiyo kila mwezi bila shida kwa mwaka utakuwa umeweka akiba ya shilingi milioni kumi na mbili.
Watu wengi wanaweza kufikiri hii ni nadharia ambayo haiwezekani, UKweli ni kuwa hiki kitu kinawezekana bila shida kabisa.
Ikiwa utahitahiji usaidizi njoo kwetu tukuelekeze namna unavyoweza kuondokana na umaskini usio wa lazima.
Kumbukeni ndugu wajasiriamali kwamba ukiamua ni kweli ndoto yako itatimia.
KARIBUNI SANA 0753903809
Kwetu tunafanya haya:
1. Tunauza mashine za kutotoa vifaranga
2. Tunauza vifaranga
3. Tunatoa ushauri

Saturday, January 3, 2015

Mwaka 2015 kwa nguvu mpya na maarifa mapya

Napenda kuwapa heri ya mwaka mpya wajasiriamali wote. Nategemea mwaka huu wajasiriamali wengi zaidi wataungana nasi katika kujikwamua na umaskini huu.
Nawashauri ndugu zanguni kufanya kazi halali kwa bidii kuliko kukaa ukiota eti kuna siku utaingiziwa fedha za ESCROW na fulani.
Kwa wale wanaotaka kuondokana na umasikini kwa njia ya ufugaji wa ndege mbalimbali kama kuku na kware tuwasiliane kwa namba hapo juu.
Mashine zetu za kuangulia vifaranga zinaendelea kutengenezwa kwa bei zifatatazo
- Incubator ya mayai 180 = Tsh 1,500,000
- Incubator ya mayai 300 = Tsh 2,200,000
- Incubator ya mayai 600 = Tsh 2,800,000
- Incubator ya mayai 1000 = Tsh 3,500,000
KARIBUNI WOTE