Saturday, July 17, 2010

UCHAGUZI MWAKA 2010

Ndugu zangu waTanzania wapenda nchi yetu, nawaombeni sana sisi sote kwa pamoja tukumbuke kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu.
Mstakabali wa nchi yetu ipo mikononi mwetu. Maendeleo ya nchi yetu yanatutegemea sisi.
Nawaombeni sana mkumbuke kuwa tunatakiwa tuchague viongozi watakaotufaa. Tunataka viongozi watakao kuwa chachu ya maendeleo. Viongozi wanaochukua chao mapema na kuondoka hatuwataki kabisa.
Mwaka huu ni wakati mwafaka wa kunyang'anya dhima ya uongozi tuliyowapa wale wote ambao hawajatekeleza yale waliyoahidi. Hivi jamani kuwa kiongozi ni kuwa bosi kwa wale walokupa dhamana hiyo?
Je, uongozi katika nchi yetu ni ya wale tu waliotuibia mali zetu na kujidai kuwa wao ndo watafutaji wazuri kuliko wengine?
Jamani mimi naomba tubalike wote kwa pamoja ili kuifanya nchi yetu isonge mbele. Mtu yeyote anaweza kuwa kiongozi ili mradi tu awe na nia ya kuwatumikia wananchi wenzake. Kuwa kiongozi maana yake kuwa na uwezo wa kuonesha njia na siyo kuwa na kujisikia bosi fulani.
Naombeni wananchi wenzangu tushirikiane kuwang'oa wale wote walotudanganya mwaka 2005 na tuwaweke wale tunaofikiri wana nia njema na nchi yetu na siyo wale mafisadi.
Tukumbuke kuwa uongozi siyo mali ya mtu binafsi.
Tarehe 31 -10 -2010 iwe ni siku ya mageuzi na isiwe ni siku ya kuwapa mafisadi ulaji.
Asanteni!