Wednesday, June 26, 2013

KARIBUNI TUSHIRIKIANE KUUONDA UMASKINI KWA KUBUNI MIRADI ISIYOHITAJI MITAJI MIKUBWA

MRADI WA KUFUGA KUKU WA KIENYEJI
Katika maisha kila mtu hutamani sana kufikia mafanikio makubwa kwa kadri anavyoweza.
Kutamani kufikia mafanikio ni hulka ya mwanadamu. Sisi Watanzania tunazo fursa nyingi sana ambazo tukizichangamkia tunaweza kufanikiwa sana na kujivunia Utanzania wetu.
Pamoja na kuwa na fursa za kujiajiri, Watanzania wengi hawana wazo la kujiajiri kama walivyo majirani zetu kama Kenya.
Kwetu sisi Watanzania uwanja ya ajira binafsi ni bado ngeni sana. Bado namba ya watu kwa mfano wanaomaliza chuo na kuwa na wazo la kujiajiri ni ndogo sana hapa Tanzania.
Hii inatokana na mfumo wa elimu tunayopata hapa kwetu. Elimu tunayoipata haimuandai mtu kuwa mbunifu vya kutosha na kuwenza kuwa na mawazo ya kuchagua ajira binafsi dhidi ya ile ya kufanya kazi serikalini au mashirika ya watu wengine.
Muda umefika kwetu sisi watanzania wa kuchagua ajira binafsi. Tukiingia huko faida ni kubwa sana maana uzalishaji utaongezeka.
Mimi binafsi nimeamua kujikita kwenye biashara ya kufuga kuku baada ya kuacha kazi serikalini. Nimeacha kazi baada ya kuona sipati muda wa kufanya kile ambacho nafikiri kingeweza kuniondoa kwenye dimbwi la umaskini. Huko nilikofanyia kazi nilikutana na watu wapo kazini zaidi ya miaka 30 lakini hawakukoma kulalamika kwamba kazi wanayofanya haikuwafikisha pale walipotegemea kufika walipoanza kazi. Nilipoona hata mimi naanza kulalamika nikaondoka haraka sana maana nilijishtukia kwamba si muda mrefu ningeungana na walalamikaji.
MJIUNGE NAMI TUFUGE
Kwa wale wanaotaka kufuga, mnaweza kununua mashine za kuangulia vifaranga kutoka kwetu na tunawenza kuwasiliana kwa namba 0753903809 au 0655903809.
Mashine zenu ni nzuri na zenye ufanisi mkubwa sana na zina guarantee. Mashine zetu ni automatic kwa maana kuwa zinasoma joto kwa digital display na hizi display ni very sensitive to temperature changes.
Mashine zetu zinageuza mayai zenyewe. Zinageuza mayai kila saa kwa maana kuwa zinageuza mayai mara 24 kwa siku na hivyo kuongeza utotolekaji wa mayai. Effficiency (ufanisi) yake ni mpaka 90% na hii ina ushahidi maana tunakuruhusu kuwatembelea wafugaji ambao tayari wana mashine zilizonunuliwa kwetu.
KARIBUNI SANA. SISI TUNAPATIKA IRINGA MANISPAA