Wednesday, July 1, 2015

UFUGAJI WA KUKU KWA FAIDA NA TIJA

Wajasiriamali wengi hupenda miradi ambayo huwaletea matokeo au faida mapema,
Mradi wa kufuga kuku ni mradi ambao huleta faida kwa muda mfupi sana.
Ili upate faida kubwa ni vizuri ukawa na mradi ambao unaweza kuumudu kwa kuwa na mahitaji muhimu katika mradi wako.
MFANO, mtu anayetaka kufuga kuku tuseme 500 anatakiwa kuwa na vifaranga 550. Awe ana uwezo wa kuwalisha hao vifaranga na kuwapa tiba. Pia awe na uwezo wa kujenga banda bora.

 Baada ya hapo kinachotakiwa ni umakini wa kufuatilia mradi katika kipengele cha utoaji huduma kwa kuku hao. Katika kundi hilo la kuku 500, 50 wanatakiwa kuwa majogoo na 450 mitetea.
Katika hao mitetea 450 aslimia 75 wanatakiwa watage kila siku. Asilimia 75 ya 450 ni kuku 337. 
Mayai ya kuku hawa huuzwa kwa Tsh. 300@. Hivyo kila siku utapata Tsh 337 x 300 = Tsh. 100000.
Kama mtu anaweza kupata Tsh. 100000 kila siku kwa mwezi una uhakika angalau wa kuweka akiba ya Tsh. 100000 bila shida. Kama utaweka akiba ya fedha hiyo kila mwezi bila shida kwa mwaka utakuwa umeweka akiba ya shilingi milioni kumi na mbili.
Watu wengi wanaweza kufikiri hii ni nadharia ambayo haiwezekani, UKweli ni kuwa hiki kitu kinawezekana bila shida kabisa.
Ikiwa utahitahiji usaidizi njoo kwetu tukuelekeze namna unavyoweza kuondokana na umaskini usio wa lazima.
Kumbukeni ndugu wajasiriamali kwamba ukiamua ni kweli ndoto yako itatimia.
KARIBUNI SANA 0753903809
Kwetu tunafanya haya:
1. Tunauza mashine za kutotoa vifaranga
2. Tunauza vifaranga
3. Tunatoa ushauri