Friday, March 29, 2013

Mwongozo kwa wafugaji wa kuku wa kienyeji
Pengine umekuwa ukiwaza sana nini ufanye ili uweze kufanikiwa na kuondokana na adha za umaskini. Yako mambo mengi ya kufanya mimi nataka kukufungua macho kwa jambo moja tu tena kwa uchache. Jambo hili anaweza kulifanya mwenye mtaji mkubwa au mdogo.Viko vitabu vingi na tena siku hizi zinatolewa DVD za jinsi ya kufanikiwa katika maisha. Utashangaa mpaka unamaliza kusoma au kutazama DVD hizo hujapata njia ya wazi sana sana utajilaumu tu kwa kuendelea kupoteza fedha kwa kuchangia miradi ya wajanja hao. Wengine wanakuambia "amini tu kuwa wewe ni tajiri na utafanikiwa" mh! INAWEZEKANA? Afadhali hao, balaa zaidi ni wale ambao wanayanadi mafanikikio na utajiri kwa mizizi, hirizi na hata roho za binadamu wenzao!

Somo langu ni dogo lakini naamini wapo watakaopata mafanikio makubwa sana. Sasas kuwa makini zaidi. Unaweza kuanza kwa mtaji wa Mil.1 mpaka laki tano au hata chini ya hapo. Mfano. Unaweza kutumia Tsh 250,000 kununua kuku 25 kwa bei ya Tsh 10,000 kwa kuku mmoja (kadirio la juu) Majogoo watakuwa 5 kwa uwiano wa 1:4 . Hii ina maana kuwa wakishaanza kutaga utakuwa na vifaranga 20 x 10 = 200 Watunze vizuri. Wale vifaranga tunakadiria kuwa makoo(majike) watakuwa 150 ambao ndani ya miezi 3 au zaidi nao wataanza kutaga. Utakuwa na kuku 200 + 25 =225 ndani ya miezi 6. Miezi 6 inayofuata 225 - (majogoo 55) = 170 Hii ina maana kuwa 170 x 10= 1,700. Ndugu mwanajamvi hayo niliyotoa ni makadirio ya chini sana hivyo mpaka mwisho wa mwaka utakuwa na kuku zaidi ya 2000. Mwaka utakaofuata utakuwa na kuku wangapi baada ya kuuza kuku 1,000. Mwaka 2. 750(majike) x 10 = 7500 (uza wengine) 3000 x 10 = 30,000. Kutegemea na uwezo wako mpaka mwisho wa mwaka wa pili utakuwa umefanikiwa sana. Kumbuka huu ni mwongozo tu, fanya utafiti na ufuatilie zaidi huku ukiacha kando uzushi wa vitabu vya wasanii na DVD zao pia. NB. Kumbuka kuku ninao wazungumzia hapa ni wale wa kawaida sio wale mataahira (wa kisasa).Fuatilia zaidi kuhusu matibabu na matunzo mengineyo.MAELEZO ZAIDI
UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJISEHEMU YA KWANZA

UTANGULIZI

Napenda kumshukuru mwenyezi Mungu ambaye ameniwezesha kwa namna moja au nyingine kutoa mchango wangu kwa mtindo huu. Huu ni kama mwongozo tu wa nini utakabiliana nacho au unatakiwa kufanya katika zoezi zima la ufugaji wa kuku wa kienyeji. Nimeamua kuuleta kwenu wana JF ili kwa mtu mwenye malengo ya kufanikiwa kupitia ufugaji wa kuku ajue mlolongo mzima na changamoto ambazo atakabiliana nazo.

A.KWA NINI KUKU WA KIENYEJI?

1. Wastahimilivu wa magonjwa lakini ni muhimu wakikingwa na magonjwa ya kuku kama mdonde, ndui ya kuku n.k ili kuweza kuwaendeleza.
2. Wana uwezo wa kujitafutia chakula ardhini.
3. Wana uwezo wa kuatamia mayai, kutotoa na kulea vifaranga na ustahimilivu wa mazingira magumu kama ukame, baridi n.k
4.Nyama na mayai yake vina ladha nzuri kuliko kuku wa kisasa.(PATA SUPU YA KUKU WA KIENYEJI ILI UTHIBITISHE)
5. Wana uwezo wa kujilinda na maadui kama mwewe n.k . Pamoja na sifa hizi ni muhimu muhimu kuku hao wakapewa matunzo mazuri, wakawekwa kwenye mabanda mazuri, wakapewa maji na chakula cha kutosha.

B.FAIDA ZA KUKU WA KIENYEJI.

Faida ni nyingi na zinafahamika lakini nitaeleza zile ambazo kwa wengine huenda zikawa ni ngeni kwao.
- Mayai huweza kutumika kwa tiba. (Pata maelezo jinsi yai la kuku wa kienyeji linavyoweza kutumika kwa tiba kutoka kwa wataalam wa tiba mbadala)
- Kiini cha njano cha yai kinaweza kutumika kutengenezea mafuta ya nywele (shampoo)
- Manyoya yake yanaweza kutumika kama mapambo.
Fuga kuku upate faida kwa kuzingatia:
Chanjo ya mdondo kila baada ya miezi mitatu na chanjo ya ndui mara mbili kwa mwaka
Zuia viroboto, utitiri na minyoo.
Chagua mayai bora kwa ajili ya kuatamiza
Panga kuuza kuku kwa makundi uongeze kipato
Kula mayai na kuku kadri uzalishaji unavyoongezeka.
Kipato unachokipata utenge pia na kiasi kwa ajili ya uendelezaji wa kuku

C:MAPUNGUFU

Yako mapungufu mengi yanayofahamika lakini hapa naomba niweke lile la muhimu zaidi. MAGONJWA kama mdondo na ndui huathiri ufugaji wa kuku kutokana na kutokuzingatia kuchanja kuku kwa wakati.


D: KABILA ZA KUKU WA KIENYEJI

Kuna maelezo ya kusisimua sana kuhusu makabila ya kuku wa kienyeji, hata hivyo kuna ugumu kidogo kuweza kuyachanganua makabila hayo kutokana na muingiliano mkubwa wa vizazi kati ya aina mbalimbali za kuku hao. Hata hivyo kuku hawa wana tofauti za kimaumbile zinazosaidia kwa kiasi fulani kutambua uwepo wa baadhi ya makabila ya kuku. Kabila hizi pia zinahusishwa kwa kiasi kikubwa na eneo kuku wanakotoka. Baadhi ya kuku wa kienyeji wanaweza kutambuliwa kwa maumbile yao Mfano:
a. Kishingo - kuku wasio na manyoya shingoni
b. Njachama au Nungunungu - Hawa ni wale wenye manyoya yaliyosimama.
c. Kibwenzi - Ni wale wenye manyoya mengi kichwani.
d. Kibutu- Hawa hawana manyoya mkiani
Mwingiliano wa vizazi unaweza ukasababisha kuku kuwa na aina ya maumbile mchanganyiko. Mfano kuku aina ya kuchi anaweza kuwa na alama ya kishingo, Njachama, Kibwenzi au Kibutu.
Hivyo kabila za kuku zifuatazo zinaweza kutambuliwa kama ndiyo kabila za kuku wa kienyeji kulingana na maumbile yao na maeneo wanakotoka.

(i) KUCHI

Ni kuku warefu kwa umbo na wenye kusimama mgongo ukiwa wima. Wana manyoya machache mwilinini na hasa kifuani, vilemba vyao ni vidogo. Majogoo huwa na wastani wa uzito wa Kg. 2.5 na mitetea kg 1.5 mayai ya kuchi yana uzito wa wastani wa gm 45. Kuku hawa hupatikana kwa wingi maeneo ya Mwanza, Shinyanga, Tabora na Zanzibar.

(ii) CHING'WEKWE

Kuku hawa ambao jina lao ni gumu kidogo kwa mtu asiyekuwa na meno kulitamka wana sifa zifuatazo.
Majogoo wana wastani wa kg 1.6, Mitetea wastani kg 1.2, mayai wastani wa gm 37. Kuku hawa wenye umbo dogo hupatikana zaidi maeneo ya CHAKWALE mkoani Morogoro na pia sehemu za umasaini. Kuku hawa hutaga mayai mengi sana kuliko aina nyingine ya kuku wa kienyeji waliopo Tanzania, kwa hiyo wanafaa sana kwa biashara ya mayai.

(iii)UMBO LA KATI

Majogoo wana uzito wa wastani wa kg. 1.9, Mitetea kg. 1.1, Kuku hawa ndio hasa wanaoitwa wa kienyeji(wa kawaida) Wana rangi tofauti. Utafiti umeonyesha kuwa kuku hawa hukua upesi na hupata kinga upesi baada ya kuwachanja dhidi ya ugonjwa wa mdondo (Castle desease)
Muhimu - Mfugaji akifanya uchaguzi kutoka kwenye aina hii ya kuku na kutoa matunzo mazuri kwa hao kuku waliochaguliwa, Hakika anaweza kupata kuku walio bora na wenye uzito wa kutosha pia kutaga mayai mengi na makubwa.

(iv) SINGAMAGAZI

Ni aina ya kuku wakubwa wa kienyeji wanaopatikana zaidi TABORA, kuku hawa wana utambulisho maalum kutokana na rangi zao. Majogoo huwa na rangi ya moto na mitetea huwa na rangi ya nyuki. Uzito - Majogoo uzito wa wastani wa kg 2.9, mitetea wastani wa kilo 2 mayai gramu 56.

(iiv) MBEYA

Kuku hawa wanapatikana Ileje mkoani mbeya. Asili hasa ya kuku hawa ni kutoka nchi ya jirani ya Malawi na si wa kienyeji asilia bali wana damu ya kuku wa Kizungu "Black Australop". Majogoo Kg 3 mitetea kg 2 mayai gram 49

(iiiv)PEMBA

Hupatikana zaidi Pemba. Majogoo Kg.1.5 Mitetea Kg 1 mayai wastani gm 42

(xi) UNGUJA.

Majogoo Kg 1.6,mitetea kg 1.2 mayai gm 42. Kuku hawa wa Unguja na Pemba wanashabihiana sana na Kuchi isipokuwa hawa ni wadogo.


SEHEMU YA PILI

1. MIFUMO YA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI.

A. MFUMO HURIA
Katika mfumo huu kuku huachiwa wakitembea toka asubuhi wakijitafutia chakula na maji na kufungiwa kwenye vibanda visivyo rasmi wakati wa usiku. Huu ni mfumo rahisi lakini si nzuri kwa mfugaji wa kuku wengi kwani atahitaji eneo kubwa la ardhi.

FAIDA.
Mfumo huu una faida za gharama ndogo za uendeshaji kiujumla.

HASARA
Uwezekano mkubwa wa kuku kuliwa na vicheche, kuibiwa mitaani n.k
Kuku huweza kutaga popote na kusababisha upotevu mkubwa wa mayai.
Ni rahisi kuku kuambukizwa magonjwa
Utagaji unakuwa si nzuri kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Uwekaji kumbukumbu si nzuri.
Ni vigumu kugundua kuku wagonjwa hivyo kusababisha ugumu katika utoaji wa tiba.

UTUMIAJI NZURI WA MFUMO HUU
Kuku wajengewe banda kwa ajili ya kulala nyakati za usiku na liwasaidie wakati mwingine wowote hali ya hewa inapokuwa si nzuri.
Kuku wapatiwe chakula cha ziada na maji.
Kuku waandaliwe kwa viota vya kutagia.
Kuku 100 ni vizuri wakitumia eneo la ardhi la ekari 1.


B.MFUMO NUSU HURIA
Huu ni mfumo ambao kuku hujengewa banda rasmi na banda hilo huzungushiwa uzio/ wigo. Mfumo huu ni ghari kiasi ukilinganisha na mfumo huria lakini huweza kumpatia mfugaji faida haraka sana.

FAIDA
Sehemu ndogo ya kufugia hutumika kuliko ufugaji huria, utunzaji wa kuku ni rahisi ukilinganisha na mfumo huria, Ni rahisi kutibu magonjwa ya mlipuka kama mdondo (Newcastle desease), Upotevu wa kuku na mayai ni mdogo sana ukilinganisha na mfumo huria.


C. MFUMO WA NDANI
Kuku hujengewa banda rasmi na hufugwa wakiwa ndani. Mfumo huu kuku huwekwa kwenye mabanda ambayo sakafu hufunikwa kwa matandiko ya makapi ya mpunga, takataka za mbao(randa), maganda ya karanga au majani makavu yaliyokatwa katwa.

FAIDA
Mfumo huu unahitaji eneo dogo la kufugia, uangalizi mzuri na rahisi wa kuku, Joto litokanalo na matandiko lina uwezo wa kuua vimelea vya maradhi, kuku wanakingwa na hali ya hewa mbaya na maadui wengine.

HASARA
Uwezekano wa kuku kudonoana ni mkubw na pia Gharama za ujenzi wa mabanda

UTUMIAJI MZURI WA MFUMO HUU.
1. Matandiko yageuzwe kila siku
2. Kila mara matandiko yawe makavu kwa kuwa na madirisha yanayopitisha hewa ya kutosha, ambayo yatatoa unyevunyevu hewa chafu ikiwemo ammonia.
4. Mita mraba moja hutosha kuku 5 hadi 8.UTATUZI WA KUKABILIANA NA VIKWAZO KATIKA UFUGAJI.
Mambo ya kuzingatia:

Mabanda bora - Fuatilia kwa wataalamu wa mifugo walio karibu nawe.
Sifa za banda bora (Waone wataalam wa mifugo)
Kuchagua kuku wa kuendeleza kizazi
Kuwa makini na aina ya mitetea na majogoo unatakiwa kuchagua ili kuwa na kizazi bora.


UTAGAJI WA MAYAI
Kwa kawaida kuku huanza kutetea(Kutoa mlio wa ishara ya kutaga) anapofikisha miezi sita hadi minane. Hivyo ni vyema viota viandaliwe mapema wakiwa na umri wa miezi mitano. Kuku anapoanza kutaga akifikisha mayai matatu mfugaji anashauriwa kuondoa kila yai linalozidi hayo matatu kila siku linapotagwa na kuliweka alama ya tarehe au namba kwa kutumia penseli ili kumfanya kuku aendelee kutaga kwa lengo la kufikisha mayai 15 mpaka 20. Mayai yanayoondolewa yawekwe kwenye chombo kikavu kinachopitisha hewa ni vizuri pia kuweka mchanga ndani ya chombo hicho.

Hakikisha ya fuatayo.
Sehemu iliyochongoka iwe chini na pana iwe juu.
Hifadhi sehemu yenye hewa ya kutosha na isiyohifadhi joto
Mayai yasikae kwenye hifadhi hiyo zaidi ya wiki mbili toka siku ya kuanza kutagwa.

UATAMIAJI WA MAYAI NA UANGUAJI WA VIFARANGA
Uatamiaji na uanguaji wa kubuni - Mfumo huu hutumia mashine za kutotoleshea vifaranga (Incubators) hutumika kuangua mayai mengi kati ya 50 hadi 500 kwa wakati mmoja Mashine zinazotumika kutotoleshea vifaranga wa kisasa zinaweza kutumika pia kutotoleshea wa kienyeji.
Uatamiaji na uanguaji wa asili

KUCHAGUA MAYAI YA KUANGUA.
Hili nalo ni muhimu kuzingatia. Ni vizuri kuchagua mayai ya kuatamia ili mayai yasiyofaa yaweze kuuzwa au kutumiwa nyumbani kwa chakula. Mayai ya kuatamia yawe na sifa zifuatazo
Yasiwe na uchafu yawe masafi
Yasiwe na nyufa
Yatokane na kuku aliyepandwa na jogoo
Yasiwe madogo wala makubwa bali yawe na ukubwa wa wastani kulingana na umbile la kuku.
Yasiwe mviringo kama mpira pia yasiwe na ncha kali sana.
Yasiwe yamekaa muda mrefu zaidi ya wiki mbili toka yalipotagwa
Yasiwe yaliyohifadhiwa kwenye sehemu yenye joto.

KUMTAYARISHA KUKU WA KUATAMIA
Pamoja na matayarisho hayo zingatia kumuwekea mayai yasiyozidi 15 pia ni vizuri yasipungue 12. Kuku wanaotazamiwa kuatamia ni lazima wachunguzwe kwa makini kabla ya kuatamia ili kuhakikisha kwamba hawana chawa, utitiri n.k. Kuwepo kwa wadudu hao huwafanya kuku wakose raha na kutotulia kwenye viota vyao. Hali hii husababisha kuanguliwa kwa Vifaranga wachache.
Sasa unatakiwa kufanya yafuatayo:-
Nyunyiza dawa ya kuua wadudu ndani ya kiota
Pia mnyunyuzie dawa kuku anayetarajia kuatamia
Weka mayai kwenye kiota huku mikono yako ikiwa imepakwa jivu ili kuepuka kuwa na harufu kwani kuku anaweza kuyasusa.

Ni vizuri kuifanya kazi hii ya kumuandaa kuku anayetaka kuatamia wakati wa usiku. Pia ifahamike kuwa kwa kawaida kuku huatamia mayai yake siku 21.

PIA JIFUNZE MBINU ZA KUATAMIA MAYAI MENGI KWA NJIA ZA ASILI
Iwapo una kuku wengi wanaotaga kwa wakati mmoja ni vema ukawafanya wakaatamia na kutotoa pamoja.
Unachotakiwa kufanya ni kuchagua mayai ya kuatamia ukianzia na yai la mwisho kutaga.
Unaweza kuwaandaa kuku wako zaidi ya mmoja ili waanze kuatamia kwa pamoja na kupata vifaranga vingi kwa mara moja kuku wa kwanza anapoanza kuatamia. Mwekee mayai viza au ya kuku wa kisasa kwani kuku huatamia hadi mayai yanapoanguliwa hivyo ukimuwekea mayai yasiyo na mbegu atakaa hapo muda mrefu hadi vifaranga watoke.

UTEKELEZAJI WAKE
Kuku anapotaga kila siku weka alama ya namba au tarehe kulinganisha na siku anayotaga
Yanapofika mayai matatu yaondoe na muwekee mayai viza au ya kisasa huku ukiendelea kuweka alama mayai yanayotagwa kila siku.
Mara kuku anapoanza kuatamia muongezee mayai ya uongo yafikie 8 hadi 10
Fanya hivyo kwa kila kuku anayetaga hadi utakapoweza kupata idadi itakayoweza kukupatia vifaranga wengi kwa wakati mmoja.
Wawekee kuku wote mayai siku moja kwa kuondoa mayai ya uongo na kuwawekea mayai ya ukweli wakati wa usiku.

MUHIMU
Mayai ya kuatamia yasishikwe kwa mkono ulio wazi na wala yasipate harufu za mafuta ya taa, manukato n.k.

JIFUNZE PIA KUTAMBUA MAYAI YALIYO NA MBEGU NA YALE YASUYO NA MBEGU.
Mfugaji anaweza kutambua mayai yaliyo na mbegu na yale yasiyo na mbegu siku ya saba baada ya kuanza kuatamia iwapo atapima mayai kwa kutumia box lililotengenezwa maalum pamoja na tochi yenye mwanga mkali ndani ya chumba chenye kiza. Hii itamuwezesha mfugaji ayatumie mayai yasiyo na mbegu kwa chakula cha familia au kuyauza.

TAMBUA VYAKULA NA UZALISHAJI WA KUKU - Sitalielezea hili naomba ufuatilie mwenyewe.

JIFUNZE MBINU ZA KUZALISHA KUKU WENGI KWA MUDA MFUPI
Zoezi hili linawezekana iwapo uleaji wa vifaranga kwa njia ya kubuni utatumika. Kuku mmoja anaweza kutotoa zaidi ya mara saba kwa mwaka.
Taz.
Hesabu ya uzalishaji wa kuku wengi kwa mwaka kwa kutumia mtetea mmoja tu.
Mpaka mwisho wa mwaka unaweza kuwa na idadi ya vifaranga 252 kwa kadirio la vifaranga 8 kila mzao. Hivyo kama una kuku 10 wanaotunzwa vizuri utakuwa umezalisha jumla ya vifaranga 2520.

Fuatilia kwa wataalamu wa mifugo ili ufundishwe zaidi kuhusu mbinu hiyo ya kuzalisha kuku wengi.

ULEAJI WA VIFARANGA
NJIA YA KUBUNI
NJIA YA ASILI
Njia zote mbili zinafahamika kama huzifahamu tafadhali fuatilia kwa mtaalamu aliye karibu nawe.


MAGONJWA NA WADUDU WANAOSHAMBULIA KUKU WA KIENYEJI NA JINSI YA KUKINGA.

A. MAGONJWA.
Ugonjwa hatari - Mdondo/ Kideri (Newcastle desease) Hapo nyuma dawa ya kukinga ugonjwa huu ilikuwepo lakini ilikuwa inahitaji kuhifadhiwa kwenye hali ya ubaridi (Friji) Hali hiyo ilisababisha iwe ngumu kutumika vijijini kwa dawa hiyo. Hivi sasa kumepatikana chanjoa ambayo inastahimili joto ambayo inaweza kutumika hata vijijini.

Pamoja na mdondo yapo pia magonjwa yanayoshambulia kuku hapa nchini

Ndui ya kuku(Fowl pox)
Mafua ya kuku(Infectious coryza)
Homa ya matumbo (Cocciodiosis)
Minyoo na wadudu kama viroboto, chawa, utitiri na kupe wa kuku.

DALILI ZA KUKU MGONJWA.

Huzubaa
Hali chakula/maji vizuri
Hujitenga na wenzake
Hujikunyata au kuinama
Hutetemeka
Hutembea kwa shida
Utagaji wa mayai hupungua au hukoma kabisa


MAGONJWA YA KUKU HUSABABISHWA NA NINI?
Yako mambo mengi yanayosababisha lakini matunzo hafifu pia huchangia.

ATHARI ZA MAGONJWA.
Hili liko wazi

Maelezo haya ya magonjwa ni mengi hivyo tuwe wafuatiliaji kwa wataalam.MATIBABU

KIDERI - Sifahamu tiba ya kitaalam ya ugonjwa huu kama kuna ambaye anafahamu tunaomba atufahamishe lakini ziko dawa za asili na za kitaalam ambazo zinafaa zaidi kwa chanjo.
Ugonjwa huu unaweza kuukinga kwa kuwapa kuku chanjo ya Mdondo. Pia usichanganye kuku wako na kuku ambao huna taarifa zao za chanjo.

KUMBUKA
Mdondo au kideri ni ugonjwa tishio ambao huweza kuua kuku wote
Mdondo ukitokea vifo huwa vingi pia kuku hupumua kwa taabu, hupooza na wengine huzunguka na huzungusha vichwa.
Mdondo unaweza kuzuilika kwa chanjo kila baada ya miezi 3

NDUI YA KUKU
HOMA YA MATUMBO (Fowly typhoid)
MAFUA YA KUKU(Infectious coryzya)
KUHARISHA DAMU(Coccidiosis)
Minyoo na wadudu wanaoshambulia kuku kama viroboto n.k

Kwa magonjwa na wadudu tuliowataja hapo juu please wasiliana na mtaalamu wa mifugo aliye karibu nawe Kwani siwezi kueleza kila kitu hapa wataalamu tunao naamini watatusaidia.

TIBA ZA ASILI
Kuna madawa ya asili ambayo hutokana na mimea ambayo hukinga kuku.

BAADHI YA MIMEA INAYOTIBU NA KUKINGA MARADHI YA KUKU.

MWAROBAINI - Typhoid, kuhara, kideri, kifua na vidonda
ALOEVERA - Typhoid, kuhara, kideri, kifua na vidonda,ngozi na Cholera. Tutaelekezana zaidi namna ya kuandaa dawa hii.

Hapa nataka niorodheshe baadhi ya madawa ya asili ambayo yanasaidia kutibu na kukinga kuku.
Mwarobaini, Aloevera, Mtakalang'onyo(Euphorbia),Mbarika, mlonge, Ndulele/dungurusi/tura/ndura, Majani ya mpapai, Mwembe, Minyaa na Pilipili kichaa.

NAWASHUKURU PIA NAOMBA MWENYE MCHANGO ZAIDI AENDELEE KUONGEZEA

Sifa, Faida na Changamoto za Ufugaji wa Kuku wa Asili
Kuku wa Asili ni wale ambao wamekuwepo hapa nchini kwa miaka mingi na damu yao
haijachanganyika na ya kuku wa kigeni. Kuku hawa wana rangi na maumbo mbali mbali.
Idadi ya kuku wa Asili hapa Tanzania inakadiriwa kufikia milioni 56. Kati ya kaya milioni 3.8
zinazojishughulisha na kilimo nchini, kaya milioni 2.3 hujishughulisha na ufugaji wa kuku wa asili.
Kwa kawaida ufugaji wa kuku wa Asili hapa nchini kwetu Tanzania hufanywa na wafugaji wadogo
wadogo wanaoishi kando kando ya miji na wale wanaoishi vijijini. Kuku hawa hufugwa huria (freerange),
yaani hufungiwa ndani nyakati za usiku na hufunguliwa asubuhi ili wajitafutie chakula.
Kuku hawa hutoa mazao machache sana yaani nyama na mayai, kwa mfano kuku mmoja hutaga
kiasi cha mayai 40-60 kwa mwaka badala ya 100-150 iwapo atatunzwa vizuri. Pia uzito wa kuku
hai ni wa chini sana, wastani wa kilo 1.0–1.5 katika umri wa zaidi ya miezi 6 badala ya kilo 1.8–2.5
iwapo atatunzwa vizuri.
Sifa za Kuku wa Asili:
Wastahimilivu wa magonjwa, lakini ni muhimu wakikingwa na baadhi ya magonjwa ya kuku
kama mdondo, ndui ya kuku nk. ili kuweza kuwaendeleza.
Wana uwezo wa kujitafutia chakula ardhini, lakini ili kuwaendeleza ni lazima kuwapa chakula
bora cha ziada.
Wana uwezo wa kuatamia mayai, kutotoa, kulea vifaranga na ustahimilivu wa mazingira
magumu (ukame, baridi nk).
Nyama na mayai yake vina ladha nzuri kuliko kuku wa kisasa.
Kwa kiasi fulani wana uwezo wa kujilinda na maadui kama vile mwewe.
Pamoja na sifa hizi ni muhimu kuku hao wakapewa matunzo mazuri, wawekwe kwenye mabanda
mazuri na imara, pia wapewe maji na chakula cha kutosha.Faida za Ufugaji wa Kuku wa Asili:
Chakula – nyama ya kuku na mayai hutumika kama chakula muhimu cha wanadamu, chenye
protini.
Chanzo cha kipato – mkulima hupata fedha akiuza kuku au mayai.
Chanzo cha ajira – ufugaji wa kuku hutoa ajira kwa jamii.
Kuku hutumika kwenye shughuli za ndoa kama vile kutoa mahari na pia ni kitoweo muhimu
katika sherehe hizo.
Gharama nafuu za kuanzisha na kuendesha mradi huu.
Ni kitoweo rahisi na chepesi kwa wageni kuliko wanyama wakubwa kama ng’ombe au mbuzi.
Ni kitoweo kisichohitaji hifadhi, hutumika mlo mmoja au miwili na kumalizika.
Kuku na mayai hutumika kwa tiba za asili.
Jogoo hutumika kama saa anapowika nyakati za alfajiri na majira mengine ya siku.
Hutuhabarisha iwapo kiumbe kigeni au cha hatari kwa mlio maalum wa kuashiria hatari.
Mbolea – kinyesi cha kuku kinaweza kutumika katika kurutubisha mashamba ya mazao na
mabwawa ya samaki.
Kuendeleza kizazi cha kuku wa asili hapa nchini.
Soko lipo la uhakika, ukilinganisha na kuku wa kisasa kwani nyama na mayai yake hupendwa
zaidi na walaji.
Manyoya ya kuku hutumika kama mapambo, pia huweza kutumiaka kutengenezea mito ya
kulalia na kukalia.
Shughuli za utafiti – kuku wanatumika katika tafiti nyingi za baiolojia, kama kutambua mambo ya
lishe.
Shughuli za viwandani:
Mayai yenye mbegu ya jogoo hutumika katika kutengeneza dawa za chanjo.
Magamba ya mayai yanaweza kutumika katika utengenezaji wa vyakula vya wanyama.
Kiini cha njano cha mayai kinaweza kutumika kutengeneza mafuta ya kuoshea nywele
(shampoo).
Mapungufu ya Kuku wa Asili:
Hutaga mayai madogo wastani wa gramu 47 ambapo kuku wa kisasa wastani wa gramu 55,
aidha hutaga mayai machache wastani wa mayai 60 kwa mwaka ambapo kuku wa kisasa
huweza kutaga hadi mayai 300 kwa mwaka.
Ukuaji taratibu – kuku wa asili hukua taratibu kutokana na lishe duni. Kutokana na hali hiyo kuku
huchukua muda mrefu (miezi sita) kufikia uzito wa kuchinjwa (kilo 1 - 1.5). Hali hii pia hufanya
faida ya ufugaji wa kuku wa asili kuchukua muda mrefu kupatikana.
Nyama yake ni ngumu (huchukua muda mrefu kuiva) ikilinganishwa na kuku wa kisasa.
a.
b.
c.
d.
e.
f.
g.
h.
i.
j.
k.
l.
m.
n.
o.
p.a.
b.
c.
Changamoto katika ufugaji kuku wa asili:
Mabanda: Ukosefu wa mabanda bora.
Wezi, wanyama na ndege hushambulia kuku.
Magonjwa: kama mdondo na ndui huathiri ufugaji wa kuku.
Tabia na miiko ya baadhi ya jamii. Baadhi ya jamii za makabila hapa nchini huona ufugaji wa
kuku kama ni kitu duni.
Upatikanaji haba wa chanjo za magonjwa kama vile, mdondo, ndui, homa ya matumbo.


Tuesday, March 12, 2013

MASHINE ZA KUANGULIA VIFARANGA VYA KUKUIli mayai ya kuku yaweze kuanguliwa kunahitajika kuwe na mambo matatu muhimu:
1.       Joto linalotakiwa kwa ajili ya kuangulia mayai
2.       Uvukevuke unaohitajika ili mayai yasipoteze maji mengi mno wakati wa kuatamiwa
3.       Mayai kugeuzwageuzwa angalau mara tatu kwa siku na zaidi ya hiyo mara tat uni vizuri zaidi.
Kwa asili kazi hizo hufanywa na mama kuku akiwa ameatamia mayai yake kwa ufanisi mkubwa sana. Tatizo linaloletwa na utaratibu huu kwa mfugaji ni kuwa mara nyingi kuku huatamia mayai machache tu kwa wakati mmoja. Kwa mfugaji wa kuku anayetaka kufuga kibiashara mfumo huu si mzuri kwa kuwa  mfugaji atapata vifaranga wachache tu tofauti labda na idadi inayotakiwa.
Ili kuondoa shida hii, mashine ambazo hufanya kazi ya mama kuku. Mashine hizo zina uwezo wa kutoa :
1.       Kutoa jito linalotakiwa kuangua vifaranga
2.       Unyevunyevu (humidity) unaotakiwa
3.       Kugeuza mayai mara nyingi kwa kadri inavyotakiwa
Sisi tunatengeneza mashine hizo ambazo zinaitwa incubators. Mashine hizo ni automated kwa maana ya kuwa hufanya kazi hizo zote zenyewe. Hii inasaidia kumpunguzia mfugaji kazi ya kuangalia mayai muda ambao mayai hayo yapo kwenye kiatamizi.
Tunatengeneza mashine za ukubwa tofautitofauti. Mashine hizo zina uwezo wa mayai kutoka 300 hadi 2000.
Kama unahitaji mashine ndogo zaidi ya mashine ya mayai 300 basi tunaweza  kukutengenezea na kama unahitaji mayai mengi zaidi ya 2000 nayo pia tutakutengenezea.
Kwa kuwa wateja wetu wengi wameonesha kuhitaji mashine za mayai machache pia kulingana na kiasi cha ufugaji wao, tumeanza kutengeza mashine za mayai 90, 120, 120, 150, 180, 210, 240, na 270n pia.
TUWASILIANE KWA: 0753903809, 0655903809
Au kwa e-mail zifuatazo:
expecamdu@ymail.com
au tembelea hapa:
KARIBUNI SANA.
Sisi tupo Iringa.

Friday, March 8, 2013

USING EGG INCUBATORS TO HATCH CHICKENSCHOOSING THE RIGHT EGGS
First, you should consider the chickens responsible for fertilizing and laying the eggs. The eggs should come from healthy adult chickens that have a high fertility percentage, were not disturbed during mating season, were fed on a good diet, and are not related to each other.
Examine the eggs. They should also be of a regular shape and average size, not larger or smaller than a typical egg produced by your chickens. Their shells should display no holes or cracks because such damage could encourage disease organisms to penetrate the egg. With this same concern in mind, you should not wash or wipe the egg, as you could remove the egg's natural protective coating that guards against such organisms.
The eggs should also be cared for correctly before incubation. This will help ensure a productive hatch. To care for the chicken eggs:
  • Store eggs in a cool, humid area, ideally 12.1 Degrees Centigrade with 75% humidity.
  • Store eggs with the large end up.
  • Turn eggs daily, use an X and 0 marking system to keep track.
  • Eggs can be stored for up 10 seven days.
  • Allow cool eggs to warm up to the ambient temperature where the egg incubator is located before putting them into the incubator.
USING THE EGG INCUBATOR
Using an egg incubator correctly will ensure the best possible success rate when hatching chicken eggs.
When hatching chickens, once the best eggs have been selected, the next step is to incubate the eggs.
An incubator is a device the mimics the environment chicken eggs would experience under a hen. The incubator keeps the eggs uniformly moist and warm, the most important conditions to consider when hatching chicken eggs. Maintaining the proper conditions within the incubator will increase the number of eggs that will actually hatch after the incubation period, about 21 days.
Proper Incubator Conditions for Chicken Eggs
When an incubator is purchased, it will come with instructions. However, knowing what conditions are ideal beforehand will help guarantee successful hatching. Temperature and humidity must be monitored daily. When setting up the incubator, the following steps should be taken before placing the eggs inside:
1. The incubator should be turned on' and brought up to temperature at least 24 hours prior to adding eggs. The incubator should be kept at around 37.6 degrees Centigrade.
2. For days 1-18, the air should be about 58-60% humid. After day 18, the humidity should be raised to 65%.You may use a Hygrometer placed inside the incubator to measure the humidity.
Chicken Egg Incubation Days 1-18
After the incubator has reached the proper temperature and humidity levels, place the eggs inside.
Besides keeping steady temperature and humidity, the most important thing to do when the chicken eggs are incubating is to turn them daily for the first eighteen days. Turning the eggs makes sure the chicks do not stick to the membrane on the side of the egg wall as they develop. If they do get stuck, they could be deformed or could drown in the liquid inside the egg when hatching. Ideally, they should be turned four to six times a day, but two to three times works well. It is best to turn them an odd number of times a day.
Mark an X on one side of all of the eggs, and an 0 on the other side to easily see which eggs need to be turned. When turning the eggs, use only clean hands to avoid infecting the eggs.
Chicken Egg Incubation after Day 18
On day eighteen of the incubation period the egg turning of the eggs should stop. Turning the eggs after eighteen days could inure the chicks.
At this point, the humidity of the incubator should be raised. The lid of the incubator should then be closed and the eggs should not be touched for the rest of the incubation period.
While waiting for the eggs to begin to hatch, the brooder box should be prepared to house the chicks until they are old enough to be outside on their own. A cardboard box lined with either newspapers or sawdust will work well. A heat lamp should be set up to shine directly into the box. The best temperature to keep the brooder box is 35 degrees Centigrade.
The chicks will begin to peep inside the eggs at about day twenty-one. It could take them up to 24 hours to fully hatch. During this time, the chicks will pull the egg yolk into their stomachs. Do not help the chicks out of their shells because the yolk could break, causing them to bleed to death. After a chick is fully hatched, let it dry completely in the incubator before removing it and placing it in the brooder box. It will most likely take several days for all of the eggs to hatch. Plan to open the incubator only once a day to remove dry chicks to avoid chilling the ones that are still damp. They will not starve to death if they remain in the incubator for a day because the yolk sustains them for three days.
After day 25, if there are still eggs that have not hatched, they should be removed and thrown away. The eggs were either unfertile or the chicks died before they could hatch. Before reusing the incubator it should be thoroughly cleaned and dried.