Friday, September 3, 2010

TUNADANGANYANA SANA

               Habari ndugu zangu Watanzania wenzangu mliopendelewa kwani  mmejaliwa maliasili nyingi sana na MWENYE-MUNGU. Hivi zamani hapo wakubwa zetu walipokuwa bado wapo shule walipokuwa wanafanya kazi za mikono huko shuleni walipungukiwa au walipata maarifa zaidi?
Siku hizi watoto wakifundishwa kazi za mikono shuleni wanasema wanaonewa maana wanasema hawakufika shule kufanya kazi za mikono,
             Lakini pia wakiachwa wasome, hawasomi maana wanaishia kusema wanatafuta "credit". Ndugu zanguni, naomba sana tukae chini tuone ni aina gani ya kizazi tunataka kujenga. Tujiulize ni maarifa gani tungependa tupate.
Mimi nafikiri mtoto anapomaliza darasa la saba awe na uwezo wa kuzalisha shambani au katika sekta yoyote anayo bahatika kuwa nayo. Kama tutaacha watoto hawa wamalize shule wakati hawaelewi hata namna ya kutengeneza mahali pa kupanda sukuma wiki, tunatengeza bomu la nyuklia.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

No comments: