Monday, September 13, 2010

KUMBE TUAMKE

  Zamani sana nilifikiri kila anayegombea uongozi ni mtu anayetaka kutumikia wananchi. Sasa ni mtu mzima nimeelewa kuwa watu wengi wanagombea uongozi kutafuta maslahi binafsi.
  Kwa mtu wa kawaida inakuwa ngumu kuingia akilini kwamba mgombea anakuja na kuahidi kufanya mambo fulani katika kipindi chake cha uongozi, lakini anapopata haonekani tena mpaka siku atakapoona siku za uongozi wake zinafika ukingoni.
  Ndugu, nchi hii ni yetu. Tuamke tuchague viongozi wanaoweza kutupeleka kule tunakotaka kwenda! Hatuwataki viongozi walafi, wanaotaka kulimbikiza mali wakati wananchi wanakufa njaa, wanakosa elimu, huduma za afya na mengineyo!
TUAMKE!!!!

No comments: