Wednesday, September 22, 2010

NCHI YETU

 Ndugu zangu Watanzania, wapenda maendeleo wote, mwasisi wa taifa hili walimu Julius Kambarage Nyerere alipokuwa akiwahutubia waandishi wa habari wa hapa nchini wa kigeni Machi 14, 1995, alishutumu sana serikali ya aliyekuwa Rais wa nchi wakati huo, Rais Alli Hassan Mwinyi, kwa sababu ya ufisadi na uvunjaji wa katiba ya nchi.
 Katika hotuba yake ambayo aliitoa katika hotel ya kimataifa ya Kilimanjaro, mwalimu alishutumu serikali ya mrithi wake Mwinyi kwa kufumbia macho suala la udini na ukabila, na kudiriki kuwaasa Watanzania kuwa makini katika kuchagua serikali mpya ambapo ilikuwa imesalia miezi saba tu kufikia uchaguzi mkuu.
 Mwalimu aliendelea kuonya kuwa ikiwa Watanzania watakubali kuendekeza udhaifu wa aina hii, basi muungano wetu utakuwa hatarini na kupelekea kutetereka kwa amani nchini.
 Aliwatatahadharisha Watanzania kwamba wamchague mtu mwenye uwezo wa kurekebisha mambo, na kuirudisha nchi katika mstari ulionyooka.
 Je, Watanzania wenzangu, leo sisi tunasemaje? Mambo yote yapo swari? Kama kuna shida yoyote, basi huu ni muda mzuri wa kutumia kura yako kuondoa kasoro yoyote katika uongozi unaofuata sasa. Tuwanyime kura wote wale ambao ni wabinafsi, mafisadi na wasiowatakia mema Watanzania.Leo hii mwalimu angekuwepo angesema mengi zaidi maana nchi yetu sasa imetumbukia kubaya.
 Mijadala bungeni imejaa masuala ya ufisadi. Mafisadi hawa tumewachagua sisi wenyewe. Mimi nafikiri hakuna haja tena ya kuchagua watu wanaonuka uchafu huo.

No comments: