Friday, September 3, 2010

SIFA ZA ANAYETAKIWA KUTUONGOZA WATANZANIA

Ndugu zangu, hivi ni zipi sifa za kiongozi tunayemtaka?
Mimi nafikiri kiongozi anayetakiwa Tanzania ni yule anayetanguliza maslahi ya wananchi mbele. Siyo yule anayefikiri kulimbikiza mali wakati wananchi wake wanahangaika.
Ndugu wananchi wenzangu, hivi sisi ni vipofu kiasi kwamba tunaweza kumchagua mtu kwa sababu labda wakati wa kukampeni alikuja na ngoma za kienyeji au palikuwa na mdundiko? Hapana, sisi si vipofu kiasi hicho! Macho yetu yasiwe kifuani, yawe kichwani.
Kwani mnataka nani awaongoze? Si yule aliyefanya mengi kuwatetea wanyonge! Hivi ndugu zangu kuna haja sana ya kuambiwa nani kavulunda na nani kaonekana anaweza akafanya zaidi?
Ombi langu kwa Watanzania wapenda nchi yao, ni kuchagua viongozi wachapa kazi watakao tetea maslahi yetu siyo wanaojaza matumbo yao bila kujali wengine wanakufa au wanaishi maisha ya ajabu sababu tu miundombinu ya uchumi hairuhusu maendeleo.

No comments: