Sunday, June 22, 2008

HIVI NDIVYO YALIVYO BUNGENI

Ndugu mhariri,Nafurahi kupata nafasi hii ili niandike kidogo kile ninachokiona katika bajeti iliyosomwa bungeni wiki jana.Bajeti hii imezingatia nini.Mimi nafikiri bajeti hii haikuzingatia maslahi yoyote ya Mtanzania maana inaonekana waziri mwenyewe alisoma kitu asichokifahamu mpaka pale wapinzani walipo mshtua kuwa anachosoma si kile alichokuwa amewapa katika vitabu walivyopewa wabunge kabla.Nafikiri hakukuwa na umakini wowote wakati wa maandalizi ya bajeti hiyo. Wabunge walio wengi ni wavivu hata hawapitii kuisoma waielewe ndio wapige kura za kuunga mkono bajeti hiyo. Wabunge wengi husubiri siku ya kuunga mkono bajeti waunge mkono wa "ndio mzee" ili mambo yaishe. Hawajali maslahi ya wapiga kura wao. Hii inaonekana pale mbunge wa viti maalumu anapopewa nafasi ya kuchangia halafu anasimama na kusema mbunge mwenzake ameongea kwa mbwembwe wakati umma wa Watanzania wanaona amewatetea.Mimi nafikiri Watanzania tuache kushabikia vitu tusivyovifahamu vizuri maana hali hiyo inafanya serikali itumie umbumbumbu wetu kupanga bajeti inayo mbana Mtanzania wa kawaida na kumnufaisha aliye nacho tayari.Hivi serikali inatumia kale kaaya kwenye Biblia kanakosema "Aliye nacho ataongezewa na asiye nacho atanyang'anywa hata alicho nacho?".Nashauri serikali ipange mipango inayosaidia wananchi walio wengi maana wamo katika nchi yao. Ni kweli kwamba kuna kikundi kidogo kinachofaidika na nchi hii. Pia wabunge waache ushabiki usio na maana wakae chini wachambue mambo kwa makini ndipo wapige kura ya kuunga mkono hotuba ya bajeti. Nasema hili maana ninao uhakika kuna wabunge wachache sana ambao wanaelewa maana ya kimaisha iliyomo katika bajeti hiyo.

No comments: