Saturday, June 14, 2008

DUNIA TUNAKWENDA WAPI?

Ndugu zangu, dunia hii ni yetu wote. Kwa sasa Tanzania hii watu wanafikiri wenyewe ni zaidi kuliko wengine. Hii hali inaonekakana wakati watu wanapofanya mambo ya ajabu utafikiri ni wao tu wapo katika sayari hii. Watu wanajichukulia na kujilimbikizia mali bila kufikiri wengine wanapata mgao gani. Watu wanatembea kwenye mashangingi wakati wengine wanatembea kwa miguu kilomita na kilomita kwa miguu. Watu wanamwaga chakula wakati wengine wanakufa kwa njaa. Watu wengine wanakaa katika maghorofa ya mabilioni wakati wengine hawana mahali pa kukaa au wanakaa katika nyumba zinazovuja!
Watanzania wenzangu, tujaribu kuwa watu wenye kufikiri. Ukweli ni kwamba raslimali zote tulizopewa na Mwenyezi Mungu ni zetu wote. Hawa wanaojilimbikizia mali nyingi bila mpango wanaiba. Kwa mpango huo kama hawa ni viongozi hawatufai kabisa maana wao hufikiri ni bora kuliko binadamu wenzao. Hawatufai, hawatufai kabisa.
TUSIWACHAGUE TENA.
LET'S BE CONSIDERATE FOR OTHERS.

No comments: