Ili mayai ya kuku yaweze kuanguliwa kunahitajika kuwe na
mambo matatu muhimu:
1.
Joto linalotakiwa kwa ajili ya kuangulia mayai
2.
Uvukevuke unaohitajika ili mayai yasipoteze maji
mengi mno wakati wa kuatamiwa
3.
Mayai kugeuzwageuzwa angalau mara tatu kwa siku
na zaidi ya hiyo mara tat uni vizuri zaidi.
Kwa asili kazi hizo hufanywa na mama kuku akiwa ameatamia
mayai yake kwa ufanisi mkubwa sana. Tatizo linaloletwa na utaratibu huu kwa
mfugaji ni kuwa mara nyingi kuku huatamia mayai machache tu kwa wakati mmoja.
Kwa mfugaji wa kuku anayetaka kufuga kibiashara mfumo huu si mzuri kwa kuwa mfugaji atapata vifaranga wachache tu tofauti
labda na idadi inayotakiwa.
Ili kuondoa shida hii, mashine ambazo hufanya kazi ya mama
kuku. Mashine hizo zina uwezo wa kutoa :
1.
Kutoa jito linalotakiwa kuangua vifaranga
2.
Unyevunyevu (humidity) unaotakiwa
3.
Kugeuza mayai mara nyingi kwa kadri inavyotakiwa
Sisi tunatengeneza mashine hizo ambazo zinaitwa incubators.
Mashine hizo ni automated kwa maana ya kuwa hufanya kazi hizo zote zenyewe. Hii
inasaidia kumpunguzia mfugaji kazi ya kuangalia mayai muda ambao mayai hayo
yapo kwenye kiatamizi.
Tunatengeneza mashine za ukubwa tofautitofauti. Mashine hizo
zina uwezo wa mayai kutoka 300 hadi 2000.
Kama unahitaji mashine ndogo zaidi ya mashine ya mayai 300
basi tunaweza kukutengenezea na kama
unahitaji mayai mengi zaidi ya 2000 nayo pia tutakutengenezea.
Kwa kuwa wateja wetu wengi wameonesha kuhitaji mashine za
mayai machache pia kulingana na kiasi cha ufugaji wao, tumeanza kutengeza
mashine za mayai 90, 120, 120, 150, 180, 210, 240, na 270n pia.
TUWASILIANE KWA:
0753903809, 0655903809
Au kwa e-mail zifuatazo:
expecamdu@ymail.com
au tembelea hapa:
KARIBUNI SANA.
Sisi tupo Iringa.
2 comments:
me nataka kuanza biashara ya kufuga kuku.but nataka kujua thamani halisi ya mashine ya kuangulia vifaranga uwezo wa mayai 90.ni shilingi ngapi na kwa kana ya kaskazini mnapatikana wapi?
Tuwasiliane kwa simu 0753903809
Post a Comment