Tuesday, December 18, 2012

MASHINE ZA KUANGULIA VIFARANGA VYA KUKU, BATA NA NDEGE WENGINE
:
Ili mayai ya kuku yaweze kuanguliwa mambo yafuatayo huhitajika:
1.       Joto linalohitajika (37.5C0)
2.       Kugeuzwa angalau mara tatu
3.       Unyevunyevu unaohitajika
Mambo hayo matatu yakiwepo, mayai ya kuku huwenza kuanguliwa baada ya siku 21. Kuku waataminzi huweza kufanya kazi hii kwa ufanisi mkubwa sana.
Tatizo la kuku waataminzi ni kuwa huwenza kuatamia mayai machache tu kwa muda mmoja. Hivyo ili mfugaji aweze kupata vifaranga wengi kwa pamoja ni lazima awe na kuku waataminzi wengi sana.
Kuondokana na shida hii, watu hutumia mashine ziitwazo “incubator” ambazo hufanya kazi badala ya mama kuku.
Faida ya kutumia incubator ni kuwa mfugaji hupata vifaranga wengi kwa pamoja. Mashine hizi zina uwezo mkubwa sana wa kutotoa vifaranga. Sisi Watanzania ndio tupo mwanzo kabisa wa kujenga utayari katika uzalishaji wa mazao kibiashara.
Sisi tunatengeneza mashine za aina mbalimbali na kwa ukubwa tofauti kama zinavyoonekana hapa chini.
Mashine hizi ni “automated” kwa maana ya kuwa:
1.       Huweka joto kwa kiwango kinachotakiwa zenyewe
2.       Huweka unyevu (humidity) unaotakiwa zenyewe
3.       Hugeuza mayai mara nyingi itakiwavyo zenyewe.
Kwa wale wanaozihitaji mfike Iringa mjini au kama mko mbali tunaweza kuwafikishia  hizo mashine mpaka mahali mlipo bila wasiwasi.
Tunatengeneza mashine za mayai 90, 120, 180, ... mpaka 1000.
Tuwasiliane kwa:
0753903809 au
0655903809
au
na kwa maelezo zaidi tembelea www.mrmduda.blogspot.com na tunaweza kuchat kwenye skype ukitembelea kwenye website hiyo na pia tunaweza kuonana kwenye facebook.
MNAKARIBISHWA WOTE.1 comment:

Gabriel Frank said...

mnapatikana mkoa gani?