Wednesday, November 17, 2010

NYERERE FUFUKA UONE MAFISADI WAMEPOKA NCHI

Kwanza tuomba kuwasalimia Watanzania wenzangu!
Kwa kweli, naomba niyaseme yaliyomo moyoni mwaka maana nchi yetu inapelekwa kubaya.
Nakumbuka enzi hizo za utawala wa mzee Mwinyi kuna mambo yalitaka kujitokeza mwalimu akayakemea kwa nguvu zake zote. Leo yanatokea hakuna mtu wa kuyakemea. Wanyonge wasio na mtetezi wamebaki wanalia. Mafisadi wamekosa huruma,. Rushwa kila mahali.
Kwanza, Watanzania tujue kuwa matokeo ya uchaguzi yaliyotoka yanasemekana siyo yenyewe na kweli dalili zipo kwamba si yenyewe. Matokeo yamechakachuliwa na hivyo wananchi wamenyang'anywa haki ya kumchagua kiongozi wanayemtaka. Kama hali ndo hii ndugu zangu Tanzania yetu inaenda wapi?
Pili, Tanzania hakuna huduma inayotolewa bila kuwa na harufu ya rushwa. Popote unapoenda kupata huduma lazima uwe na chochote. Bila hivyo hakuna anayekujali. Watu sasa wanajali matumbo yao tu! Ubinafsi unatuua. Uongozi uliopo unaona lakini hakuna kinachosemwa kuhusu hayo mambo. Angalia wakati wa uchaguzi watu walitoa hela hadharani na hakuna aliyechukuliwa hatua maana watwala wenyewe walihusika. Uongozi umenunuliwa na wwatu wenye pesa na kama huna mfukoni shauri yako kafie mbali.
Tatu, udini umekuja kwa kasi ya ajabu. Watu sasa hawachagui viongozi kulingana na hoja walizo nazo wagombea ila huyu anasali wapi na ni muumini wa dini gani. Angalia wakati wa uchaguzi watu walivyohamasishana kuchagua waumini wenzao badala ya kuangalia kiongozi anayefaa. Tanzania leo hakuna mtu wa kukemea haya wazi wazi. Viongozi wakubwa wastafu hawana hata ubavu wa kukemea lakini wanayaona. Chukua mfano CCM walipokuwa wanafungakampeni zao rais mstaafu Benjamin William Mkapa alivyokanusha kuwepo kwa masuala ya udini wakati yapo kabisa na yanaonekana. Halafu mzee huyo aliwakandia viongozi wa dini kwa kusema kuwa wenyewe ndo wanaleta udini. Hiyo si kweli ila viongozi wakubwa wa kisiasa wameonesha kwa vitendo kabisa udini walio napo. Angalia teuzi mbalimbali za viongozi, mwelekeo ni udini haswa lakini mtu akisema eti ni mzushi. Jamani, nawaambieni nchi hii inakoenda siko. Tuchukue hatua. Demokrasia inaminywa.
Nne, kwa sasa ukiwa mtetezi wa wanyonge hapa Tanzania unaonekana hufai. Angalieni kilichotokea kwa mheshimiwa spika wa zamani wa bunge Sitta. Kwa kweli inasikitisha maana unapoona mzee kama yule aliyejitoa kuhakikisha bunge linakuwa mtetezi wa maslahi ya taifa anaonekana hafai tena, nani anfaa sasa? mafisadi wa nchi hi ndo wanafaa? Mimi nasema ujinga wetu Watanzania unatumaliza kabisa!
Tano, angalieni viongozi wastaafu wanasema nini. Kimya!! Mwalimu alipostafu alibaki kuwa mshauri, hivyo hata kama kuna jambo lilionekana kwenda visivyo, alikemea. Leo nani akemee maana akiona ananyamaza kwa kuwa usafi wake unatiliwa mashaka. Kwani nyie Mafisadi mnataka muwe naTsh ngapi ndugu zanguni? Mnasahau kuwa maisha hapa duniani hayazidi miaka mia moja? Kwa kweli MUNGU SAIDIA!!
Sita, ukionekana umejitokeza kutaka kusaidia maskini na watu wakikukubali, mafisadi wanakuja juu! Mafisadi wanataka kuendesha serikali. Jamani, mimi nalia. Tufanye nini ndugu zanguni! Mwalimu tunaomba ufufuke utusaidie tumebanwa kila kona! Hatuwezi kupumua!! Mfano, Dr. Slaa anaonekana kuja na mbinu mbadala kwa ajili ya kurekebisha hizi taabu za maisha wanazopata Watanzania. Baada ya kuona hivyo mafisadi wamekuja na kila uchafu wa kumbebesha mtu huyu! Hivi ina maana Tanzania uongozi ni wawateule fulani? Mbona mtu akitokea kuonekana anataka kuwashinda mnatumia mbinu chafu hata uongo wa kuzua ilimradi wananchi wamchukie? Ndugu, nchi hii imetekwa na mafisadi. Maskini hatuna chetu. Wattoto wa viongozi wanazunguka huku na huku wakitumia raslimali za wananchi ili mradi tu wazazi wao washinde kwenye chaguzi waendelee kula paradiso ya dunia!
Mwisho, enyi ndugu zangu Watanzania, mbona mmelala? Watu mliofikiri mnachagua wawakilishe, hawasimamii hoja zenu! Wakipewa cheo wanafanya kazi kwa maslahi ya wale waliowaweka. Hawaangalii maslahi ya watu. Mfano, hivi kulikuwa na sababu gani ya spika wa bunge kuanza kutoa tafsiri ya uongo ya neno "fisadi". Eti anafanya hivyo ili kumdhalilisha mtu fulani. Na kosa la mtu huyo tu ni kwa kuwa alitaka kunyang'anya kitumbua mdomoni mwao! Hivi ni lini hawa watu watawawakilisha wananchi. Majitambo yao eti wamekuwa uongozini toka miaka ya sabini. Bila aibu wanafikiri watu wanawashangilia na kufurahi. Miaka hiyo yote mmeoipeleka wapi nchi yetu hii? Jamani Watanzania tufanye nini hapa? Wabunge wetu wanampigia kura mtu ati kwa kuwa wako chama kimoja na siyo hoja alizonazo! Hivi hawa wabunge wetu wanafaa kweli? Watatusaidia nini. Malengo yao ni kusaidia watu au kuhakikisha wanalinda nafasi na kuongezewa nafasi nyingine kwa kuwalamba miguu viongozi wa chama chao!! Inatisha.
TUNATAKA MABADILIKO!!!
0753903809

No comments: