Ndugu Watanzania wenzangu wapendwa, duniani hapa tupo ili kuhakikisha maisha yanaendelea bila matatizo yoyote.
Shida zinazojitokeza na kutufanya tuishi kwa shida zimeletwa na sisi wenyewe.
Ili kuhakikisha kila mmoja wetu anashiriki kupanga namna vile angependa kuishi kwenye nchi hii aliyopewa na Mwumba wake, ni vema kila mmoja wetu ashiriki kikamilifu kutoa maoni kuhusu katiba mpya ya nchi yetu.
Kwa Tanganyika, huu ndo mwaka pekee ambao tunapata wasaa wa kuirudisha nchi yetu Tanganyika na tukizubaa tu basi katiba itakayokuja itatufanya tuishi kwa kugugumia kwa miaka mingine hamsini.
Mimi napendelea kati ya haya:
1: Tuwe na serikali moja ya Tanzania
2: Kama 1 ni ngumu, basi tuwe na serikali tatu, yaani serikali ya Tanganyika, serikali ya Zanzibar na serikali ya Muungano.
0753903809
BLOG YA UJASIRIAMALI:UFUGAJI WA KUKU: KWA MAHITAJI NA USHAURI WA UFUGAJI WA KUKU NA MASHINE ZA KUANGULIA VIFARANGA VYA KUKU TUWASILIANE KWA NAMBA 0753903809 AU 0655903809